ANKARA : Mripuko wauwawa wanajeshi watatu
10 Juni 2007Matangazo
Hali ya mvutano ni kubwa kusini mashariki mwa Uturuki baada ya askari watatu kuuwawa na mripuko wa bomu lililotegwa barabarani nje ya mji wa Sirnak.
Serikali ya Uturuki imewalaumu waasi wa Kikurdi kwa shambulio hilo ikiwa ni masaa machache tu baada ya serikali ya Iraq kuvishutumu vikosi vya Uturuki kwa kushambulia kwa mabomu kutoka mpakani hadi ndani mwa kaskazini mwa Iraq na kusababisha hasara kubwa.
Uturuki imeongeza wanajeshi wake mpakani na Iraq katika wiki za hivi karibuni wakati viongozi wa nchi hiyo wakijadili iwapo wawaandame waasi wanaotaka kujitenga wa Kikurdi kwa kumvuka mpaka wa Iraq.