ANKARA: Mwito kufunga kambi za waasi wa Kikurd
20 Oktoba 2007Matangazo
Waziri Mkuu wa Uturuki,Reccep Tayyip Erdogan ametoa mwito kwa Baghdad kufunga kambi za waasi wa Kikurd kaskazini mwa Irak.Serikali ya Ankara imeitaka Irak iwasalimishe Uturuki,viongozi wa chama cha Kikurd cha PKK kilichopigwa marufuku Uturuki.
Siku ya Jumatano,bunge la Uturuki liliidhinisha ombi la serikali kupeleka majeshi yake upande wa pili wa mpaka wake na Irak ya kaskazini kuwasaka waasi wa Kikurd wanaolitumia eneo hilo la mpakani kuishambulia Uturuki.
Baghdad na Washington zimetoa mwito kwa Uturuki kutotumia nguvu za kijeshi,kwa hofu kuwa hatua hiyo huenda ikasababisha machafuko katika eneo la utulivu,kaskazini mwa Irak.