1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ankara. Uturuki haiingii umoja wa Ulaya, iwapo chama cha CDU kitashinda uchaguzi.

27 Agosti 2005

Kansela Gerhard Schröder wa Ujerumani amesema kuwa ushindi wa chama cha upinzani katika uchaguzi mkuu ujao hautakuwa na mwelekeo mzuri kwa Uturuki na kuwataka wapinzani hao kutimiza ahadi iliyotolewa kwa Uturuki ya kuwa mwanachama kamili katika umoja wa Ulaya.

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Ujerumani Angela Merkel , akiwa anaongoza katika kura ya maoni kabla ya uchaguzi hapo Septemba 18 , amewataka viongozi wa vyama vya kihafidhina katika umoja wa Ulaya kuipa Uturuki nafasi ya mshirika mpendelewa, badala ya mwanachama kamili wa umoja huo.

Bwana Schröder ameliambia gazeti la Uturuki la Hurriyet kuwa kuingia madarakani kwa chama hicho cha upinzani hakutakuwa na manufaa kwa Uturuki, na kuwataka wanasiasa wa Ujerumani kutimiza ahadi iliyotolewa kwa Uturuki kujiunga na umoja wa Ulaya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW