ANKARA : Wanajeshi wa Uturuki waachiliwa huru
5 Novemba 2007Matangazo
Waasi wa chama cha wafanyakazi wa Kikurdi PKK wamewaachilia huru wanajeshi wanane wa Uturuki waliowateka wiki mbili zilizopita katika shambulio karibu mpaka wa Uturuki na Iraq.
Wanajeshi hao wanane wamekabidhiwa maafisa wa Kikurdi wa Iraq ikiwa ni siku moja baada ya serikali ya Iraq kuapa kuchukuwa hatua dhidi ya waasi wa Kikurdi wanaoishambulia ardhi ya Uturuki kutoka makambi yao yalioko kaskazini mwa Iraq.
Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan leo anatazamiwa kukutana na Rais George W. Bush wa Marekani mjini Washington kujadili mzozo huo.Erdogan alisema kabla ya kuondoka kwake kuelekea Marekani kwamba anatumai mazungumzo hayo yatapeleka kuchukuliwa kwa hatua madhubuti kudhibti kundi hilo la PKK lilioko Iraq.