ANKARA: Wanamgambo wa PKK watashambuliwa zaidi
17 Julai 2006Matangazo
Uturuki imearifu kuwa inafikiria kuimarisha mapigano yake dhidi ya waasi wa Kikurd.Tangazo hilo limetolewa baada ya hadi wanajeshi 7,mlinzi mmoja wa kijijini na afisa mmoja wa polisi kuvamiwa na kuuawa na wapiganaji wa chini kwa chini.Chama cha Wakurd cha PKK kilichopigwa marufuku,kinagombea mamlaka ya kujitawala kusini-mashariki mwa Uturuki ambako wakaazi wengi ni wenye asili ya Kikurd.Serikali mjini Ankara imesema kuwa mashambulio ya hivi karibuni yaliyoua watu 14 tangu siku ya Alkhamis, yalifanywa kutoka kaskazini mwa nchi jirani ya Irak.