ANKARA:EU kufungua sura mpya ya uanachama wa Uturuki
4 Juni 2007Umoja wa Ulaya unapanga kufungua sura mpya kuhusu uanachama wa Uturuki lakini kuishawishi kufanya mageuzi ya kudumisha demokrasia kwa madhumuni ya kufanikiwa.Waziri wa Mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier ana imani kuwa mazungumzo kuhusu masuala ya Uchumi na sera za fedha,takwimu na usimamizi bora wa fedha yataanza tarehe 26 mwezi huu baada ya uchaguzi kufanyika tarehe 22.
Uturuki imelazimika kusogeza mbele uchaguzi kutoka mwezi Novemba kufuatia mkwamo wa kisiasa baada ya Waziri wa mambo ya nje Abdullah Gul aliye na misingi ya kiislamu kushindwa kuteuliwa mara mbili baada ya kuwa mgombea pekee wa wadhifa huo.Upinzani ulisusia uchaguzi huo.
Umoja wa Ulaya unapanga kufungua sura mpya kuhusu uanachama wa Uturuki lakini kuishawishi kufanya mageuzi ya kudumisha demokrasia kwa madhumuni ya kufanikiwa.Waziri wa Mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier ana imani kuwa mazungumzo kuhusu masuala ya Uchumi na sera za fedha,takwimu na usimamizi bora wa fedha yataanza tarehe 26 mwezi huu baada ya uchaguzi kufanyika tarehe 22.
Vural Öger ni mbunge wa chama cha SPD katika Umoja wa Ulaya aliye na asili ya Uturuki.
GO TO AUDIO
ÖGER O TON
Kwa njia yoyote iwayo Uturuki inalazimika kufuata misingi ya Sheria za Umoja wa Ulaya iwapo itakuwa mwanachama au la.Kwa sehemu kubwa suala la kufuata misingi ya sheria hizo limekuwa kubwa na taifa la Uturuki linataraji mageuzi makubwa ambayo yanatokana na misingi ya Umoja wa Ulaya.