ANKARA:Gul aapishwa kuwa rais wa Uturuki
29 Agosti 2007Matangazo
Abdul Gul ameapishwa kuwa rais wa 11 wa Uturuki.
Katika hotuba yake baada ya kuapishwa aliahidi kuendeleza kanuni za taifa lisiloegemea dini.
Gul aliapishwa hapo jana saa chache baada ya kushinda duru ya tatu ya uchaguzi katika bunge.
Wapinzani wa bwana Gul ikiwa ni pamoja na jeshi la nchi hiyo wamezungumzia mashaka yao kuhusu sifa zake za kuwa na siasa ya kidini katika miaka ya nyuma.Kansela wa Ujerumani Anngela Merkel amempongeza Gul kwa kuchaguliwa rais.Merle amesema katika barua yake ya pongezi kwamba anaimani nchi hizo mbili Uturuki na Ujerumani zitaendelea kudumisha uhusiano wao wa karibu na kushirikiana kwa pamoja katika masuala mbali mbali.