ANKARA:Wanachama 15 wa PKK wauwawa Tunceli
29 Oktoba 2007Jeshi la Uturuki limesema limewaua kiasi cha wapiganaji 15 wa kikurdi wakati hali ya wasiwasi ikiendelea kusini mashariki mwa Uturuki.
Wapiganaji hao waliuwawa katika opresheni kali iliyofanywa na wanajeshi wa Uturuki kwenye mkoa wa Tunceli ulioko mbali na Iraq.
Uturuki imepeleka wanajeshi wake zaidi ya laki moja karibu na mpaka wa Iraq tayari kwa uwezekano wa kuwashambulia waasi wa chama cha wafanyikazi wa kikurdi cha PKK kaskazini mwa Iraq.
Mapigano ya hapo jana yametokea kabla ya mazungumzo muhimu kati ya Uturuki na Marekani kuhusu mzozo huo yaliyopangwa kufanyika wiki hii.Mzozo huu umeitumbukiza Marekani katika hali isiyoyakawaida hasa ikizingatiwa nchi zote mbili Uturuki na Iraq ni washirika wake. Waziri wa mambo ya nje wa Iraq Hoshyar Zebari ameilaumu Uturuki kwa kukosa nia ya kutaka kuutatua mzozo huu kwa njia ya amani.