1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA:Ziara ya Kansella Gerhard Schroeder Uturuki

4 Mei 2005

Kansella wa Ujerumani Gerhard Schroeder nchini Uturuki ameitaka nchi hiyo kutekeleza mageuzi ya kisiasa yatakayoiwezesha kufikia kanuni za Umoja wa Ulaya.Kansella Schroeder akizungumza baada ya mkutano na waziri mkuu wa Uturuki Racep Tayyip Erdogan mjini Ankara alisema hatua hiyo ni muhimu ili kuhakikisha kwamba mazungumzo juu ya kujiunga Uturuki kwenye Umoja wa Ulaya yanaanza Oktoba kama ilivyopangwa.

Schroeder pia aliunga mkono pendekezo la Uturuki kwa Armenia la kutaka kuundwe tume ya pamoja ya wanahistoria itakayochunguza madai ya kuhusika kwa utawala wa Ottoman nchini Uturuki katika mauwaji makubwa ya halaiki kwa Warmenia katika vita vya kwanza vya dunia.Baadhi ya wanasiasa wa Umoja wa Ulaya wamesema serikali ya Ankara lazima itatue suala hilo kabla ya kupata nafasi ya kujiunga na Umoja huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW