1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANNAN NA SYRIA-LEBANON

18 Machi 2005

UM-NY:

Katibu-mkuu wa UM Kofi Annan, anaitarajia Syria kuhamisha kikamilifu majeshi yake kutoka Lebanon kabla uchaguzi mkuu wa mwezi Mei-hii ni kwa muujibu vile alivyosema mjumbe wa UM Tereje Roed-Larsen.Bw.Larsen amearifu kwamba kuna mafahamiano ya kutosha ulimwenguni juu ya tarehe hiyo ya mwezi Mei kama ya mwisho.

rais Bashar al Assad wa Syria ameahidi kuhamisha kikamilifu majeshi yake pamoja na askari kanzu wake kutoka Lebanon.

Kikao cha pamoja kati ya Syria na Lebanon mwezi ujao wa April,kitaamua tarehe ya mwisho ya kuondolewa kabisa majeshi ya Syria nchini Lebanon.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW