1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANTANANARIVO: Rais Jacques Chirac wa Ufaransa awasili Madagascar kwa mkutano wa mataifa ya bahari ya Hindi

21 Julai 2005

Rais wa Ufaransa, Jacques Chirac, amewasili hii leo nchini Madagascar kwa ziara ya siku mbili kuhudhuria mkutano wa kilele wa kamati ya mataifa ya bahari ya Hindi, IOC. Chirac atakiwakilisha kisiwa cha Reunion, katika mkutano huo utakaohudhuriwa pia na rais wa Madagascar, Marc Ravalomanana, rais wa Comoro, Azali Assoumani, na rais wa Seychelles, James Ramgoolam.

Mkutano huo, utakaojadili maendeleo endelevu na kuendeleza utamaduni, unatarajiwa kuanza hapo kesho katika mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo. Mada nyengine zitakazojadiliwa pia ni maswala ya siasa, uchumi, biashara kati ya mataifa wanachama, vita dhidi ya ukimwi, mabadiliko ya hali ya hewa na ongezeko la idadi ya wakaazi. Viongozi pia watakutana na maofisa wa umoja wa Ulaya kandoni mwa mkutano huo.