1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUreno

Rais wa Ureno amelivunja bunge na kuitisha uchaguzi mpya

10 Novemba 2023

Rais wa Ureno Marcelo Rebelo de Sousa amelivunja bunge la taifa hilo na kuitisha uchaguzi wa mapema, siku mbili baada ya Waziri Mkuu Antonio Costa kujiuzulu na serikali yake iliyogubikwa na kashfa ya rushwa.

Rais wa Ureno Marcelo Rebelo de Sousa ametangaza kulivunja bunge la kitaifa na kuitisha uchaguzi mpya unaotarajiwa kufanyika Machi mwakani
Rais wa Ureno Marcelo Rebelo de Sousa ametangaza kulivunja bunge la kitaifa na kuitisha uchaguzi mpya unaotarajiwa kufanyika Machi mwakaniPicha: Armando Franca/AP Photo/picture alliance

Rebelo de Sousa amesema uchaguzi mpya huenda ukafanyika Machi 10. Ametoa tangazo hili, alipohutubia taifa kupitia televisheni baada ya kukutana na Baraza la Taifa linalohusisha wanasiasa wa zamani na waliowahi kuwa watu mashuhuri na baada ya mkutano na viongozi wa vyama vilivyoko bungeni siku ya Jumatano.

Antonio Costa aliiongoza Ureno tangu mwaka 2015, na kushinda kwa kishindo kwenye uchguzi wa Julai mwaka uliopita.

Alijiuzulu mara moja kufuata msako mkali wa polisi siku ya Jumanne, kama sehemu ya uchunguzi wa tuhuma za rushwa ambapo mkuu wake wa utumishi pamoja na watu wengine wanne walikamatwa, huku waziri mmoja akitajwa kama mtuhumiwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW