1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMisri

Antony Blinken amewasili mjini Jerusalem kukamilisha

30 Januari 2023

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken amewasili mjini Jerusalem leo mchana baada ya kukamilisha ziara yake nchini Misri ambako alitoa wito wa utulivu na kupunguzwa mvutano kati ya Israel na Palestina.

Israel Tel Aviv | Ankunft Antony Blinken, US-Außenminister
Picha: Ronaldo Schemidt via REUTERS

Bw. Blinken ambaye alikutana na rais wa MisriAbdel Fattah al-Sisi mjini Cairo, alizungumzia haja kwa kila upande kujizuia na ghasia na akagusia pia umuhimu wa suluhu ya mataifa mawili kwenye mzozo huo wa Mashariki ya Kati.

Soma pia:Blinken azungumza na rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi

Blinken atakutana jioni hii na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kabla ya hapo keshokuelekea Ukingo wa Magharibi kwa mazungumzo na kiongozi wa wapalestina Mahmoud Abbas.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW