Anyimwa uraia wa zimbabwe
30 Desemba 2006Matangazo
HARARE:
Serikali ya rais Robert Mugabe nchini Zimbabwe,imefungua mlango wazi kumpokonya leseni ya kuchapisha mkosoaji wake mkubwa nchini, Trevor Ncube uraia wake.Ncube anamiliki kundi kubwa la magazeti ya kibinafsi nchini humo..
Msajili mkuu wa vyombo vya habari nchini ,Tobaiwa Mudede amesema, Ncube anaechapisha gazeti la Mail na la Guardian ya Afrika Kusini,haruhusiwi kuwa na uraia wa nchi mbili kwavile yeye, ni raia wa Zambia kwa asili.
Zimbawe, hairuhusu uraia wa nchi mbili kama baadhi ya nchi nyengine.
Wachunguzi wanadai, hatua ya kuwapokonya passport wakoasiaji wa serikali huko Zimbabwe, ni dalili ya wasi wasi unaozidi na kutojiaamini kwa serikali ya Mugabe kwa jicho la msukosuko unaozidi wa kiuchumi