1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoArgentina

Argentina yanyakua ubingwa

18 Desemba 2022

Hatimae shangwe imetawala katika mitaa na miji ya Argentina baada ya kunyakua ubingwa wa kombe la dunia dhidi ya Ufaransa nchini Qatar

Titel: Fußball WM Katar | Argentinen vs Kroatien
Picha: Ulrik Pedersen/Defodi Images/picture alliance

Argentina imenyakua kombe la dunia baada ya kuilaza Ufaransa kupitia mikwaju ya Penalti 4-2.  Ufaransa iliyokuwa ikitetea kombe hilo imekosa penalti mbili na kurudi nyumbani bila kombe lakini ikiwa kifua mbele kutokana na mchezo iliyounoesha katika mpambano  huo.

Waargentina waliamka Jumapili hii wakiwa tayari kabisa kuutazama mchuano huo wa kihistoria kwao  kuwania taji hilo kwa mara ya tatu tangu mwaka 1986 huku wakiwa na mshikamano na furaha isiyokuwa ya kawaida katika taifa hilo ambalo limetumbukia katika hali ngumu ya kiuchumi kwa miaka sasa, ikiwa na mfumko mkubwa wa bei ambao ni mbaya zaidi duniani kuwahi kuonekana.

Mfumko wa bei umefikia kiasi asilimia 100 kwa mwaka na kati ya kila waargentina 10 takriban wanne wanaishi katika umasikini mkubwa.

Picha: Rodrigo Abd/AP Photo/picture alliance

Wanasema ukiitazama nchi hiyo hivi sasa ni kama ambaye soka imewakusanya sehemu moja na kuwatumbukiza wote. Mara ya mwisho Argentina kufikia fainali ya kombe la dunia ni mwaka 2014 ilipopoteza dhidi ya Ujerumani.

 

Argentina yatinga fainali Kombe la Dunia

 

Kwa ujumla WaArgentina waliotupa matarajio yao kwa nguli wao wa soka Lionel Messi wanasema walikuwa na  kiu mno ya kulinyakua kombe la dunia mwaka 2022 nchini Qatar.