1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUjerumani

Ari ya kibiashara Ujerumani yashuka kwa miezi minne

Sylvia Mwehozi
24 Septemba 2024

Ari ya biashara nchini Ujerumani imeshuka kwa mwezi wa nne mfululizo mnamo Septemba, kulingana na uchunguzi uliofanywa huku taifa hilo lenye nguvu kubwa kiuchumi Ulaya likijitahidi kujikwamua kutoka mdororo wa uchumi.

Bidhaa katika duka mojawapo Ujerumani
Bidhaa katika duka mojawapo UjerumaniPicha: Michael Bihlmayer/picture alliance

Ari ya biashara nchini Ujerumani imeshuka kwa mwezi wa nne mfululizo mnamo Septemba, kulingana na uchunguzi uliofanywa huku taifa hilo lenye nguvu kubwa kiuchumi barani Ulaya likijitahidi kujikwamua kutoka mdororo wa uchumi. Faharasi ya taasisi ya Ifo iliyofanya utafiti wa makampuni takribani 1,000 inaonyesha kuwa shauku ya biashara imeporomoka asilimia 85.4 kutoka 86.6 mwezi Agosti.

Rais wa taasisi ya Ifo Clemens Fuest amesema "uchumi wa Ujerumani unazidi kuwa chini ya shinikizo". Utafiti huo unaonyesha kuwa wafanyabiashara wengi hawaridhishwi na mazingira ya sasa ya kiuchumi na kutokuwa na matumaini zaidi kuhusu miezi ijayo. Taasisi ya Ifo inasema imani miongoni mwa makampuni katika sekta muhimu ya uzalishaji ilishuka "kwa kiasi kikubwa", hadi kiwango cha chini kabisa tangu Juni 2020. Fuest ameongeza kuwa kuna upungufu wa uagizaji bidhaa na kwamba sekta ya viwanda Ujerumani "zinatatizika".

Bidhaa katika duka mojawapo UjerumaniPicha: INA FASSBENDER/AFP

Ujerumani ambayo inaongoza kwa mauzo ya nje ilikuwa nchi pekee kubwa kiuchumi ambayo uchumi wake uliendelea kupungua mnamo mwaka 2023, lakini afueni iliyotarajiwa mwaka huu imeshindwa kupatikana huku kudorora kwa uzalishaji bidhaa kukiendelea na mahitaji ya ndani na nje ya nchi bado ni dhaifu.

Utafiti huo wa karibuni wa taasisi ya Ifo unatafsiriwa kuwa "habari mbaya", kwa mujibu wa Fritzi Koehler-Geib, mwanauchumi mkuu katika Benki ya Mikopo ya Umma KfW, na unaongeza ishara kwamba uchumi wa Ujerumani utakuwa "katika hali ya hatari" katika robo ya tatu ya mwaka.Ujerumani kufanya biashara ya nishati na Nigeria

Taasisi zinazoongoza za kiuchumi ikiwa ni pamoja na Ifo katika wiki za hivi karibuni zimeshusha matarajio yao ya kukua kwa uchumi wa Ujerumani na sasa zinatarajia kudorora kidogo kwa uchumi mwaka 2024.Wafanyakazi wa sekta za rejareja na jumla Ujerumani wagoma

Utafiti muhimu ulionyesha siku ya Jumatatu kuwa shughuli za biashara katika kanda inayotumia sarafu ya Euro zilipungua kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi saba, hasa kutokana na utendaji dhaifu katika mataifa mawili ya juu ya uchumi wa jumuiya hiyo, Ujerumani na Ufaransa. 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW