Armenia na Azerbaijan kufanya mazungumzo ya amani
28 Aprili 2023Haya yameripotiwa na shirika la habari la Urusi, TASS, lililomnukuu katibu wa baraza la usalama la Armenia. Katibu huyo Armen Grigoryan lakini hakusema ni lini, wapi au ni katika ngazi gani mazungumzo hayo yatakapofanyika.
Shirika hilo la habari la Urusi limeripoti pia kwamba, waziri wa ulinzi wa Armenia aliizungumzia hali ya Nagorno-Karabakh eneo lililoshuhudia vita mara mbili katika miongo mitatu iliyopita. Nagorno-Karabakh ni eneo linalotambulika kimataifa kama sehemu ya Azerbaijan ila limekuwa likikaliwa na karibu Warmenia 120,000.
Soma pia:Azerbaijan yasitisha mazungumzo ya amani na Armenia
Raia wa Azerbaijan ambao wanajitambulisha kama waandamanaji wa mazingira tangu Desemba 12, wameifunga sehemu ya njia ya Lachin ambayo ndiyo njia kuu ya pekee na inayopitia eneo la Azerbaijan na inayoiunganisha Armenia na Nagorno-Karabakh.