1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Armenia na Azerbaijan zaelekea kusuluhisha mvutano

16 Mei 2024

Armenia na Azerbaijan zimefikia makubaliano juu ya sehemu zinazozozaniwa za mpaka wao wa pamoja, hatua mpya ya kurejesha uhusiano kati ya mahasimu hao wa kihistoria.

Ilham Aliyev - Nikol Pashinyan - Charles Michel
Ilham Aliyev - Nikol Pashinyan - Charles MichelPicha: Dursun Aydemir/AA/picture alliance

Armenia na  Azerbaijan zimefikia makubaliano juu ya sehemu zinazozozaniwa za mpaka wao wa pamoja, hatua mpya ya kurejesha uhusiano kati ya mahasimu hao wa kihistoria.

Makubaliano kati ya mataifa hayo mawili ya eneo la Caucasus, ambayo yote yalikuwa jamhuri  za Kisovieti,  yamefungua njia ya kurejeshwa kwa vijiji vinne vya mpakani vya Azabajan vilivyotekwa na Armenia katika miaka ya 1990.

Mwishoni mwa mwezi Machi, Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan alikubali kurudisha vijiji vinne vilivyotelekezwa ambavyo Yerevan iliviteka katika miaka ya 1990.Azerbaijan yakataa kushiriki mazungumzo ya amani na Armenia

Akizungumza wakati wa mkutano wa baraza la mawaziri, leo Alhamisi, Pashinyan ametaja makubaliano hayo kama hatua muhimu ya kuimarisha zaidi mamlaka na uhuru wa Armenia.

Pashinyan alisema Armenia itajenga barabara mpya katika eneo hilo ndani ya muda wa miezi michache ijayo na walinzi wa mpaka wa nchi hizo mbili watawekwa kwenye mpaka uliochorwa upya "ndani ya siku 10 zijazo".

Armenia na Azerbaijan zilipigana vita mara mbili, katika miaka ya 1990 na mwaka wa 2020, kwa ajili ya udhibiti wa eneo la  Nagorno-Karabakh.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW