1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaArmenia

Armenia yaiomba ICJ kuiamuru Azerbaijan kuondoa vizuizi

30 Januari 2023

Armenia leo imeiomba Mahakama ya Kimataifa ya Masuala ya Haki, ICJ, kuiamuru Azerbaijan kuondoa vizuizi vya ilivyoviweka kwenye barabara muhimu kuelekea jimbo lenye mzozo baina ya mataifa hayo mawili la Nagorno-Karabakh.

Niederlande Den Haag | Europäischer Gerichtshof
Picha: Yves Herman/REUTERS

Mwakilishi wa kisheria wa Armenia ameiambia mahakama ya ICJ kuwa nchi hiyo inataka chombo hicho kiilazimishe Azerbajin iondowe vizuizi, vinavyozuia usafirishaji wa bidhaa muhimu kupelekwa kwenye eneo hilo.

Azerbaijan iliweka vizuizi kwenye barabara hiyo ikiituhumu Armenia kuitumia kupitisha silaha.

Soma pia:ICJ kuamua kuhusu mzozo wa mpaka kati ya Kenya na Somalia

Njia hiyo kuelekea jimbo la Nagorno-Karabakh imegeuka chanzo cha msuguano wa hivi karibuni kati nchi hizo mbili ambazo zimewahi kupigana vita mara mbili kuwania udhibiti wa eneo hilo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW