1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUingereza

Arsenal kufanya usajili muhimu ili kuikabili Man City

26 Juni 2023

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta anaamini kwamba klabu ya Gunners inahitaji kujiimarisha katika soko la usajili iwapo inataka kuipiku Manchester City kama mabingwa wa ligi ya Premier msimu ujao

Premier League | Mikel Arteta
Picha: Kirsty Wigglesworth/AP Photo/picture alliance

Kwa muda mrefu Arsenal ilikuwa kinara wa ligi kuu ya Premier, lakini ilishushwa baada ya wachezaji wake muhimu kupata majeraha.

City walibeba ubingwa kwa mara ya nne katika kipindi cha miaka mitano na hatimaye kubeba mataji matatu kwa kushinda kombe la FA na Ligi ya Mabingwa UIaya.

Soma pia: Arsenal watetereka tena, Man City watabasamu

Vilabu vyote viwili vinaripotiwa kuwa na ushindani wa kutaka kumsajili nahodha wa West Ham, Declan Rice, huku Arsenal wakitajwa pia kuwania kumsajili Kai Havertz kutoka Chelsea.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW