1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Arusha:Mawaziri wa Rwanda kizimbani:

11 Novemba 2003

Kesi ya Mawaziri wanne wa zamani wa
Rwanda wanaotuhumiwa kuhusika na
mauaji ya kiholela ya mwaka 1994
nchini humo imesikilizwa leo katika
Mahakama ya Umoja wa Mataifa ya
Vitendo vya Jinai vilivyofanywa
Rwanda (ICTR) mjini Arusha,
Tanzania. Mwendesha mashtaka
ameiambia Mahakama kuwa watuhumiwa
wana hatia ya kuua watu zaidi ya
millioni moja mwaka 1994. Watuhumiwa
wanakabiliwa na mashtaka ya
kuchochea mauaji, kuhusika na mauaji
ya kiholela, kutekeleza mauaji hayo
na kufanya vitendo ya jinai dhidi ya
utu. Watuhumiwa wanaohusika ni
Waziri wa zamani wa Afya, Daktari
Casimir Bizimungu, Waziri wa Huduma
za Jamii, Prosper Mugiraneza, Waziri
wa Mambo ya Nchi za Nje, Jerome
Bicamumpaka na aliyekuwa Waziri wa
Biashara, Justin Mugenzi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW