1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ARUSHA:Mayor wa zamani wa Rwanda aondolewa mashtaka ya kuhusika kwenye mauaji ya halaiki

23 Mei 2005

Mayor wa zamani nchini Rwanda aliyekuwa ameanza kutumikia kifungo chake cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia mwaka 2003 ya kuhusika kwenye mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 nchini Rwanda amepunguziwa kifungo hicho hadi miaka 45 jela na mahakama ya rufaa.Jopo la mahakimu wa mahakama ya rufaa ya Umoja wa Matifa inayochunguza kesi ya mauaji ya halaiki ya Rwanda ,wametupilia mbali mashtaka mawili yaliyokuwa yanamkabili meya huyo wa zamani baada ya kutupiliwa mbali kwa mashtaka ya kuhusika kwake kwenye mauaji ya halaiki. Kwa mujibu wa shirika la habari linalofuatilia vikao hivyo la Hirondelle uamuzi huo uliotolewa na jaji Fausto Pocar umetokana na msimamo wa Mayor Juvenal Kajeli jeli wa kuwa hapana ushahidi wowote kwamba alitoa amri kwa wanamgambo wa Inarahamwe kufanya mauaji. Kajelijeli mwenye umri wa miaka 54 alikuwa Mayor wa Mukingo katika mkoa wa Ruhengeri Kaskazini kutoka mwaka 1988 hadi 1993 na kwa mara nyingine katika mwaka 1994 ambapo kulifanyika mauaji ya halaiki.

Watu laki nane waliuwawa wengi wao wakiwa na watsusti walio wachache pamoja na wahutu waliokuwa na msimamo wa kadri waliouwawa na wahutu wenye siasa kali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW