1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je, asasi za kiraia kitishio kwa viongozi wa Afrika?

6 Agosti 2024

Ni nini vyanzo vya misuguano ambayo mara nyingi hushuhudiwa kati ya asasi za kiraia na serikali mbalimbali barani Afrika hasa kusini mwa jangwa la Sahara?

Tunesien Tunis | Rassismus gegen Menschen aus Sub-Sahara Afrika
Picha: Tarek Guizani/DW

 Suala hilo limejadiliwa kwa kina katika kongamano la asasi za kiraia ambalo limekamilika leo Kampala likihusu mapambano dhidi ya ugaidi na utakatishaji fedha.

Miongoni mwa mitazamo ya wajumbe imekuwa kwamba pale asasi hizo zinapowajibisha serikali, baadhi ya tawala huwachukulia kuwa tishio la kisiasa kwa uongozi wao. 

Wadau katika mtandao wa asasi za kiraia wamewataka raia wa mataifa ya Afrika kufahamu kwamba asasi hizo ni mhimili muhimu katika utawala na maendeleo ya nchi sambamba na serikali na sekta binafsi.

Soma pia:Asasi za kiraia zapambana na ugaidi licha ya kushutumiwa

Raia wakifahamu umuhimu huo basi bila shaka wataelewa kwa nini mara nyingi asasi hizo huandamwa na vyombo vya dola.

Uhasama kati ya serikali na asasi hizo hudhihirika pale sera na sheria vinapotungwa au kufanyiwa mageuzi ambayo huelekea kuwa vizingiti kwa asasi hizo kuendesha shughuli zao.

Mwanasheria na mwanaharakati wa haki za binadamu Onesmo Olengurumwa kutoka Tanzania anasema bado kuna sheria zinaminya uhuru wa mashirika kufanya kazi.

"Bado una sheria gumu zinazotukandamiza na kutuzuia kuwa na uhuru wa kuendesha kazi zetu tunaonekana kama wapinzani wa serikali kwa hiyo ni maadui wa serikali."

Changamoto za asasi za kiraia

Kutokana na azma la asasi za kiraia kupanga na wakati mwingine kuendesha maandamano kama njia ya kushinikiza tawala kuheshimu haki za binadamu, serikali zingine huzishuku kuwa kama vyama vya siasa vya upinzani.

Aidha vyombo vya dola hudai kwamba asasi hizo ni vibaraka wa mataifa ya kigeni ambayo huzitumia kwa ajili ya maslahi ya nchi zao na kwa hiyo si tishio tu kwa usalama wa nchi, lakini pia kuwa na uwezo wa kuchochea raia dhidi ya utawala.

Radio, chombo cha kueneza amani Kongo

04:11

This browser does not support the video element.

Dkt Richard Sambaiga ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam asasi hizo haziwezi kujiungua kufanya kazi za kisiasa hasa katika nyakati kama vile za uchaguzi ama uundwaji wa katiba.

Soma pia:HRW: Wasichana wajazito, waliojifungua waacha shule Msumbiji

"Wasiwasi mkubwa ni kwamba baadhi ya asasi za kiraia hususan zile za sekta ya utawala bora  na haki za binadamu hawezi kukwepa kuhusiana na vyama vya kisiasa au maslahi ya kisiasa."

Katika mataifa kama vile Eswatini ambapo vyama vya siasa vilipigwa marufuku, asasi za kiraia ndizo za peke ambazo hukosoa utawala. Mjumbe kutoka Nchi hiyo amefahamisha kongamano ni kutokana na hali hii ndipo serikali imezidi kubana sera na sheria dhidi ya asasi za kiraia. 

Maazimio ya asasi za kiraia

Mada kuu ya kongamano hilo la siku mbili imekuwa kujadili njia za asasi hizo kushirikiana na serikali na mashirika ya kimataifa kupambana  dhidi ya ugaidi ili kuondoa dhana kwamba fedha za kufadhili shughuli za kigaidi hupitishwa kwenye akaunti na miamala inayofanywa na asasi hizo.

Miongoni mwa mapendekezo yaliyoibuka kwenye mkutano huo ni kwamba  baada ya kutambua umuhimu wa asasi za kiraia, Umoja wa Afrika uhimize kuwepo na sera na sheria sawa zinazolinda haki za asasi za kiraia.

Vile tunavyoweza kusaidia ni kufuatilia jinsi Umoja wa Afrika unavyoendeleza mjadala huu!"

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW