1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJamhuri ya Kongo

Asasi za kiraia za pinga zoezi la kidemocrasia Kongo

16 Februari 2023

Mashirika ya kiraia katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi wa M23 Mashariki mwa Kongo wamepinga zoezi la kuandikisha wapiga kura wakitaka kuendelezwa kwa juhudi za kusaka amani badala ya kadi za kupiga kura.

DRC Wählerregistrierung in der Region Nord-Kivu
Picha: Benjamin Kasembe/DW

Hayo yanafanyika wakati hii leo mchakato wa kuandikishwa wapiga kura ukizinduliwa mashariki mwa mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, huku hali ya kiusalama katika maeneo hayo ni ya kutia shaka.

Katika tangazo lao la muda mfupi kabla ya kuanza zoezi la uandikishaji wa wapigakura, viongozi wa asasi za kiraia wamedaikuwa na hofu ya kutoendelea kwa mchakato huo kutokana na maelfu ya raia kuyakimbia makaazi yao kutokana na changamoto za kiusalama.

Soma pia:Changamoto za usajili wa wapigakura nchini Kongo

Baadhi ya raia wameiambia DW kuwa kinachopaswa kufanywa na serikali hivi sasa ni kurejesha mchakato wa amani, utakaowarejesha raia kwenye makaazi yao ya asili kabla ya mchakato wa kidemocrasia.

"Tupate amani kwenye jimbo kwanza,ili kila mtu arudi fasi yake" alisema Sengi Mbite kutoka shirika la raia wilayani nyiragongo.

Waasi watwaa maeneo ya kimkakati

Jimbo hilo ambalo ni eneo la kimkakati kwa Kongo kutokana na rasilimali mbalimbali zinazopatikana na katika eneo hilo,karibuni asilimia 80 ya jimbo limedhibitiwana waasi wanao endelea kuviteka vijiji wilayani Masisi.

Mbali na kuanza kuwahimiza wananchi kushiriki mchakato huo utakao dumu kwa takriban mwezi mmoja, baadhi ya wabunge mkoani kivu kaskazini wameonesha pia wasiwasi wao.

Soma pia:Mashirika ya kiraia yakabiliana na polisi Kongo

Mbunge wa kuchaguliwa na wananchi katika wilaya ya Beni Muhindo Celce amesema ni jambo lisilowezekana kuendelea kwa zoezi wakati maelfu ya raia wanaishi uhamishoni.

"Inaleta hofu,serikali ya Kongo inapaswa kuangalia namna gani itamaliza vita kwanza" Alisema mwanasiasa huyi anaewawakilisha wananchi ya Beni.

CENI:Tunazitambua changamoto 

Zaidi ya watu milioni 4 wanatarajiwa kushiriki zoezi hilo pamoja na vituo elfu moja vya usajili vitakavyo wapokea wananchii hao  wanaohangaishwa na vuruguu za vita.

Zoezi la kuandikisha wapiga kura likizinduliwa Kivu KaskaziniPicha: Benjamin Kasembe/DW

Jenerali Constant Ndima akiwa gavana wakijeshi kwenye mkoa wa kivu kaskazini, amesema wanatambua changamoto  zinazo wakabili raianakuahidi kuwa serikali imepanga mikakati iliyo thabiti ili kila mmoja kupata fursa ya kushiriki zoezi hilo la kikatiba na kidemocrasia.

Zoezi hili linafanyika wakati ambapo bado maelfu ya wakimbizi wa Kongo wapo katika kambi za wakimbizi ndani na nchi jirani kutokana na hali ya usalama kutotabirika.

Soma pia:Baadhi ya wakaazi wazuiwa kujiandikisha kama wapiga kura DRC

Hata hivyo katika mji wa Goma baadhi ya raia wameendelea kujitokeza kwenye vituo vya kujiandikisha huku mapigano yakishuhudiwa baina ya jeshi la Kongo na waasi wa M23 mjini Kitshangani wilayani Masisi.

Licha ya jumuiya za kimataifa kuingilia kati ili kukomesha vurugu mashariki mwa Kongo, bado kundi la M23 ambalo Kinshasa inadai linaungwa mkono na Kigali, limeendeleza mashambulizi yake na kudhibiti baadhi ya vijiji.

Mashambuli hayo ambayo mengi yamekuwa yakushtukiza yamesababisha mamiaya raia kushikiliwa na waasi, maelfu kupoteza maisha huku wengine mamilioni wakiyakimbia makaazi yao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW