1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ashton ahimiza ujumuisho

30 Julai 2013

Umoja wa Ulaya umechukua jukumu la kuwa mpatanishi katika kusaidia kurejesha utawala wa kiraia nchini Misri , umoja ambao ni chanzo kikuu cha misaada ya Misri kutoka nje.

A supporter of deposed Egyptian President Mohamed Mursi carries a Mursi poster during a protest at the Rabaa Adawiya square, where Mursi supporters are camping, in Cairo July 27, 2013. At least 70 people died on Saturday after security forces attacked supporters of deposed President Mohamed Mursi in Cairo, Muslim Brotherhood spokesman Gehad El-Haddad said, adding the toll could be much higher. REUTERS/Mohamed Abd El Ghany (EGYPT - Tags: POLITICS CIVIL UNREST)
Wafuasi wa Mursi wakiandamana usiku mjini CairoPicha: Reuters/Mohamed Abd El Ghany

Mkuu  wa  sera  za mambo  ya  kigeni  wa  Umoja  wa  Ulaya Catherine  Ashton amesema  katika  ziara  yake ya  pili  nchini  Misri  leo  kuwa amekutana  na  rais  aliyeondolewa  madarakani Mohammed Mursi na  kwamba  hali  yake  ni  nzuri  na  anauwezo  wa  kupata  habari.

Umoja  wa  Ulaya  utaendelea  na  juhudi  zake  za  upatanishi  ili kumaliza  mzozo  wa  Misri. Hayo  yamesemwa  na  mkuu  wa  sera za  mambo  ya  kigeni  wa  Umoja  wa  Ulaya  Catherine  Ashton  leo wakati  akimaliza  ziara  yake  mjini  Cairo.

Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa EU, Catherine Ashton mjini CairoPicha: Reuters

Akizungumza  pamoja  na  makamu  wa  rais  wa mpito  Mohammed ElBaradei, Ashton  amesema  kuwa  wanadiplomasia  wa  Umoja  wa Ulaya  watafika  nchini  Misri  kuendeleza juhudi  hizo.  "Nitarejea, amesema Ashton  , na  kuongeza  kuwa  ni  jukumu  la  wanasiasa wa  Misri  kufanya  maamuzi  sahihi."

Azungumza na  Mursi

Ashton  alikuwa  na  mazungumzo  ya  saa  mbili  na  Mohammed Mursi  alfajiri  ya  leo , huku  duru  zikilifahamisha  shirika  la  habari la  AFP kuwa  aliondoka  mjini Cairo kwa helikopta ya jeshi. Alikataa kusema ni wapi Mursi   anakoshikiliwa  ama kuelezea  maelezo aliyoyatoa kwake.

Alikuwa  mtu  wa  kwanza  rasmi  kuruhusiwa  kukutana  na  Mursi tangu  kuondolewa  madarakani  hapo Julai 3 na jeshi.

Rais aliyeondolewa madarakani Mohammed MursiPicha: Reuters

Ashton  alikuwa  akienda  huku  na  huko  kati  ya   makundi  mbali mbali  akisisitiza  ujumbe  wake  kwa  ajili  ya  amani, kuyajumuisha makundi  yote  yanayohusika  katika  mzozo  huo  katika  utawala wa  kiraia  wa  mpito  katika  taifa  hilo  la  Kiarabu  lenye  wakaazi wengi.

Ni jukumu  muhimu  kwasababu  kila  kundi  liko  tayari  kuzungumza nasi , sio  kwasababu  ya  mbinyo  wa  nchi  moja  ama  nyingine, ni kwasababu  tunaweza  kutekeleza  jukumu  hilo.

Msemaji  wa  ofisi  ya  mkuu  wa  sera  za  mambo  ya  kigeni  wa Umoja  wa  Ulaya  Michael Mann  amesema  kuwa  Ashton  amekuwa akiwasiliana  na  pande  nyingine  zenye  maslahi  katika  mzozo  huo na  amezungumza  mara  kadha  na  waziri  wa  mambo  ya  kigeni wa  Marekani  John Kerry.

Alipoulizwa  iwapo  Umoja  wa  Ulaya  unatumia  mbinu  gani  kuibana Misri , Mann  amesema  Umoja  wa  Ulaya  ni mtoaji  mkubwa  wa misaada  kwa  Misri, ambapo  kiasi  cha  euro  milioni  450  kilitolewa mwaka  2011 hadi  2013 kwa  masharti  maalum.

Waandamanaji mjini CairoPicha: Reuters/Mohamed Abd El Ghany

Hii  haina  maana  kuwa  kuna  mbinyo,  lakini  katika  miezi  ya  hivi karibuni hatujatoa  msaada  mkubwa  kutokana  na  kukosekana maendeleo  ya  kisiasa, Mann  amesema.

Mursi hatakuwamo katika mchakato mpya wa siasa

Akizungumza  pamoja  na  Ashton  katika  mkutano  mwingine  na waandishi  habari, makamu  wa  rais  wa  mpito  anayehusika  na masuala  ya  kimataifa  Mohammed ElBaradei  amesisitiza  kuwa Mursi hatakuwa  sehemu  ya  hatua  za  kisiasa  zinazoendelea.

ElBaradei  amesema  kuwa  kiongozi  huyo  aliyeondolewa madarakani  hatakuwa  na  jukumu  katika  hatua  za  kisiasa  za hapo  baadaye, licha  ya  kuwatolea  wito  kundi  la  Udugu  wa Kiislamu  kushiriki.

Makamu wa rais wa mpito Mohammed el-BaradeiPicha: imago stock&people

Mursi  ameshindwa   lakini  Udugu  wa  Kiislamu  unaendelea  kuwa sehemu  ya  hatua  za  kisiasa  na  tungependa  washiriki  katika hatua  za  kisiasa, amesema  ElBaradei.

Ameieleza  Misri  kuwa  inaingia   katika  "enzi  mpya",  baada  ya maandamano  ya  Juni 30  ambayo  yalisababisha  kuondolewa madarakani  kwa  Mursi  Julai 3.

Mwandishi : Sekione  Kitojo / afpe

Mhariri : Mohammed  Abdul Rahman 

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi