Asia ya Kusini yakumbwa na mafuriko na maporomoko ya ardhi
30 Novemba 2025
Zaidi ya watu 600 wamefariki kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa katika nchi za Indonesia, Thailand na Malaysia. Indonesia imeripoti vifo 435, Thailand 170, na Malaysia vifo vya watu watatu, baada ya dhoruba nadra katika Bahari ya Malacca na iliosababisha mvua na upepo mkali kwa wiki nzima.
Zaidi ya watu milioni 4 wameathirika, huku maelfu wakihamishwa na maeneo mengi kukosa mawasiliano. Timu za uokoaji zinatumia helikopta kufikisha msaada katika maeneo yasiofikika kwa urahisi.
Wakati huo huo, nchini Sri Lanka, kimbunga Ditwah kimeua watu 153 na wengine 191 hawajulikani walipo, huku zaidi ya nusu milioni wakihitaji msaada. Hali hii imeacha uharibifu mkubwa na maelfu bila makazi, huku juhudi za misaada zikiendelea kote katika eneo hilo.