1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Asilimia 40 ya mizozo ya silaha duniani hutokea Afrika: ICRC

23 Oktoba 2025

Takriban asilimia 40 ya mizozo inayohusu zana za kivita inatokea bara la Afrika.

Eneo la mpaka la Chad-Sudan 2004 | Waasi wa Vuguvugu la Haki na Usawa warejea kutoka doria (Picha ya maktaba)
Kanda ya sahel ni miongoni mwa maeneo yanayozongwa na mizozo ya silaha barani AfrikaPicha: Nic Bothma/dpa/picture alliance

Makamu Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu Gilles Carbonnier ameeleza kuwa kwa sasa, kuna takriban mizozo 50 ya silaha inayoendelea barani humo.

Hiyo inaashiria ongezeko la asilimia 45 tangu mwaka 2020 na hivyo kuiweka mizozo ya Afrika kuwa asilimia 40 ya mizozo yote ya silaha ulimwenguni.

Miongoni mwa nchi zinazozongwa na mizozo ya silaha ni kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Sudan, Mali na Niger

Bara hilo lina takriban watu bilioni 1.4, na lina utajiri wa madini na idadi kubwa ya vijana. Lakini sehemu nyingi ya bara hilo zimekumbwa na umaskini na ukosefu wa usalama.

Kulingana na Carbonnier, mizozo hiyo imesababisha watu milioni 35 kuyakimbia makaazi yao, hiyo ikiwa takriban nusu ya wahamiaji wote ulimwenguni.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW