Askari maelfu wafariki Heglig
23 Aprili 2012Wanajeshi wa SPLM waliouwa wamefikia1200 mwishoni mwa juma wakati Sudan Kusin ikidai kuwa inajiondoa katika eneo hilo. Huku ikiwa kimya kuzungumzia juu wanajeshi wake waliouwawa katika mapigano hayo ya mataifa ndugu.
Katika siku ya kumi ya umiliki wa Heglig Sudan Kusin ilidai kuwa wanajeshi wake waliofariki ni kumi tu na wanajeshi 240 wa Sudan waliwaua. Kwa hakika imekuwa vigumu kujua waliouwawa lakini kulinga na taarifa za mwanahabari kutoka shirika la Habari la Ufaransa (AFP) anasema eneo hilo lilikuwa na mili mingi ya maiti za wanajeshi wa Sudan Kusini. Huku akiwa na picha wanajeshi zaidi 100 toka Sudan wakipata matibabu mjini Khartoum.
Kulingana na taarifa za mmojawapo wa wasaidizi wa Rais Omar Al Bashir kwa Shirika la Habari la Sudan anasema idadi ya wanajeshi wa Sudan Kusini pamoja na mamluki wake waliouwawa kwa sasa wanafikia 400.
Hapo awali Sudan ikikataza kabisa vyombo vya habari katika eneo hili na jumamosi taifa hilo likasema kuwa limemaliza kazi ya kuwafurusha wanajeshi wa Sudan Kusini katika eneo lao la Heglig ambapo Sudan Kusini ilidai kuwa ni eneo lake katika mkoa wa Abyei.
Sudan Kusini iliteka eneo hilo April 10 mwaka huu kufuatiwa na madai yake ya ndege za Sudan kushambulia taifa hilo na baadae jumuiya ya kimataifa iliingilia kati mgogoro huo.
Kutupiana lawana
Ndege za kivita za Sudan zimefanya mashambulio Sudan Kusini ambapo mwanahabari wa AFP akiwa shuhuda wa hilo ameona mtoto mdogo ameuwawa kwa shambulio hilo la anga.
Kila upande unamlaumu mwenzake kwa kufanya uharibifu wa miundombinu ya eneo hili la mafuta la Heglig. Mataifa yote yanaongozwa na watawala waliowahi kuwa wanajeshi hapo awali. Rais al-Bashir aliwasili Heglig Jumatatu akiwa amevalia nguo za kijeshi. Ziara yake ni ya kwanza tangu alipotangaza Ijumaa iliopita kwamba majeshi yake yameyashinda yale ya Sudan kusini katika eneo hilo.
Rais Kiir ni miongoni mwa wanajeshi wakongwe ambapo aliteuliwa na mwanzilishi wa SPLA Marehemu John Garang. Rais Bashir amewahi kufanya kazi katika majeshi ya Misri na Sudan kwa miaka zaidi ya 20 huku akishiriki vita zaidi ya vitatu na kufikia cheo cha field Mashal.
Marais hao sio tu kila mmoja anajua uwezo na udhaifu wa mwenziwe lakini pia wanafahamu fika matokeo ya vita pale vinapotokea. Miaka ya 1980 jeshi la Sudan Kusini liliweza kupata mafunzo mazuri na vifaa vya kijeshi lakini majeshi ya Sudan yaliweza kuwashinda kwa kwa urahisi na haraka.
Sudan Kusini ina wanajeshi wengi
Majeshi ya Sudan Kusini yanakadiriwa kuwa na wanajeshi kati ya 30,000-40,000 huku baadhi ya takwimu zikiashiria idadi ya wanajeshi hao ni zaidi ya 160,000. Sudan Kusini inasemekana pia kuwa vifaa vingi na vya kisasa vya kijeshi kutoka China, Urusi, Ukraini na Iran.
Sudan kwa upande wake ina vifaa vya kivita kama vile makombora ya masafa marefu, vifaru na ndege za kivita ambapo vingine inatengeneza katika mojawapo ya kamapuni zake.
Pande hizi mbili ziliwahi kupigana vita kwa muda wa miaka 21 kabla ya kufikiwa mkataba wa amani 2005. Sudan Kusini ilijitenga na kuwa huru julai mwaka uliopita.
Mwandishi:Adeladius Makwega/AFPE
Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman