1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Askari wa kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi wa Iran auwawa

4 Januari 2023

Askari mmoja wa kikosi maalum cha Walinzi wa Mapinduzi nchini Iran (IRGC) ameuawa katika mji mkuu Tehran.

Revolutionsgarden im Iran
Picha: Vahid Salemi/dpa/picture alliance

Shirika la habari la Tasnim ambalo lina uhusiano wa karibu na kikosi hicho limeripoti hayo leo.

Afisa huyo aliyetambuliwa kwa jina Qasim Fethullahi alishambuliwa kwa risasi nne usiku wa kuamkia leo na baadaye akafariki hospitalini.

Polisi wa Iran wanachunguza kiini cha shambulizi hilo.

Hakuna taarifa za nyuma ambazo zilijulikana kuhusiana na tukio hilo ambalo Tasnim imetaja kuwa "shambulizi la kigaidi."

Tukio hilo limejiri mnamo wakati taifa hilo linafanya kumbukumbu ya kuuawa kwa aliyekuwa kamanda mwenye ushawishi mkubwa wa kikosi hicho, Qasem Soleimani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW