Askari wa Umoja wa Mataifa kuendelea kulinda amani DRC
20 Desemba 2019Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha nyongeza ya mwaka mmoja wa kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na wakati huo huo Umoja wa Mataifa umepunguza idadi ya jeshi na badala yake kuongeza maafisa wa polisi. Saumu Njama na taarifa zaidi
Azimio lililowekwa katika rasimu ya Ufaransa, ambalo pia linaweka mkakati wa kuondoka nchini humo , lilikubaliwa kwa hiari na baraza la wanachama 15.
Balozi wa Afrika Kusini Xolisa Mabhongo, akizungumza kwa niaba ya washirika watatu wa baraza la Afrika, alipongeza mpango huu na kwa kusema ni muhimu kujiondoa kwa MONUSCO kwa msingi wa mabadiliko baada ya kufikiwa mafanikio katika mkutano wao.
Kwa upande wake, mwakilishi wa Kongo, Paul Empole Losoko Elambe, amesema, "wazo la kulenga vikosi vya MONUSCO katika majimbo sita ambapo uwepo wa vikosi unadhaniwa kuwa ni muhimu sawia na ombi la serikali la kujikita zaidi katika majimbo ambayo yana kiwango cha juu cha vitisho na kupunguza uwepo wa jeshi katika maeneo ambayo sio tishio tena. "
Kikosi cha jeshi la umoja wa maifa MUNUSCO kitapunguzwa kutoka askari16,875 hadi 14,660.
Kulingana na mwanadiplomasia mmoja hatua hiyo ni "ishara nzuri" kwa ajili ya mabadiliko katika serikali mpya na kuimarishwa kwa usalama katika maeneo mengi.Vikosi vya UN vimefanikiwa kuzuia jaribio la shambulizi DRC
Katika rasimu hiyo, Baraza la Usalama linataka Sekretarieti ya Umoja wa mataifa izingatie kupunguzwa zaidi kwa kiwango cha kupelekwa wanajeshi kwa kuzingatia mabadiliko mazuri ya hali ya nchini Kongo, hasa katika mikoa ambayo inakabiliwa na tishio la vikosi vya wahalifu wenye silaha.
Rasimu hiyo pia inazingatia utafiti wa kimkakati wa kujitegemea nchni humo, uliofanywa hivi karibuni na inasema kwamba kuna haja ya kipindi cha chini cha mpito kwa takriban miaka tatu na inasisitiza hitaji la kuhamisha kazi za MONUSCO hatua kwa hatua kwa serikali ya Kidemokrasia ya Kongo.
Azimio hilo linaitaka serikali kumteua mratibu kuongoza juhudi za kudhibiti silaha na mipango ya kujumuisha kwa wapiganaji wa zamani, na kuanzisha kesi za kisheria dhidi ya wale wanaohusika na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Bajeti ya MONUSCO ni karibu dola bilioni moja kwa mwaka na Umoja wa mataifa umekuwepo kutekeleza kazi za kijeshi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa miaka ishirini.
AFP/