1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Askari wa Urusi watuhumiwa kumyanyasa kingono msichana

14 Machi 2023

Ukraine imewatuhumu wanajeshi wawili wa Urusi kumyanyasa kingono msichana mdogo wa miaka minne na kumbaka mamake mbele ya babake

Symbolbild Ukraine-Krieg: Protest gegen Vergewaltigung
Picha: Vuk Valcic/ZUMA Press Wire/ZUMAPRESS/Picture alliance

Ukraine imewatuhumu wanajeshi wawili wa Urusi kumyanyasa kingono msichana mdogo wa miaka minne na kumbaka mamake mbele ya babake hii ikiwa ni sehemu ya madai ya unyanyasaji yanayozidi kuongezeka dhidi ya wanajeshi wa Urusi zaidi ya mwaka mmoja tangu Urusi iivamie kijeshi jirani yake Ukraine.

Soma pia: Mapigano makali yaripotiwa katika mji wa Bakhmut

Kulingana na mafaili ya waendesha mashtaka kutoka Ukraine yaliyoonekana na Reuters, matukio hayo ni miongoni kwa misururu ya uhalifu wa kingono uliofanywa na wanajeshi wa Urusi kwa familia nne katika kijini cha Brovary karibu na mji wa Kiev mwezi Machi mwaka 2022.

Wizara ya ulinzo ya Urusi haikujibu maombi ya kujibu tuhuma hizo.

Waendesha mashtaka hao wamesema wakati wa jaribio lililofeli la kuuteka mji wa kiev baada ya uvamizi wa Februari 24, wanajeshi wa Urusi waliingia Brovary siku chache baadae wakaiba mali ya watu na kuwanyanyasa watu kingono.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW