Assad: Juhudi za kurejesha uhusiano na Ankara hazijafanikiwa
26 Agosti 2024Katika hotuba aliyoitoa katika bunge la nchi hiyo, Al-Assad amesema juhudi za kurekebisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili hazijakuwa na matokeo chanya licha ya nia ya dhati ya wapatanishi, akiashiria juhudi za upatanisho za Urusi, Iran na Iraq.
Kiongozi huyo ameeleza kuwa ili juhudi hizo zifanikiwe, kwanza lazima sababu zilizopelekea kuvunjika kwa uhusiano kati ya nchi yake na Uturuki zijulikane na kuondolewa.
Soma pia: Erdogan asema huenda akamualika Assad kwa mazungumzo nchini Uturuki
Uturuki ilivunja uhusiano na Syria mnamo mwaka 2011 baada ya kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria wakati Uturuki iliunga mkono waasi waliotaka kumwondoa madarakani Assad. Assad mwenye anawachukulia waasi hao kama magaidi.
Kiongozi huyo wa Syria ameweka wazi kwamba anataka wanajeshi wa Uturuki waondoke nchini mwake, ingawa hilo sio sharti la mazungumzo.