1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Assange aachiwa huru kwa dhamana

25 Juni 2024

Mwanzilishi wa mtandao wa WikiLeaks Julian Assange ameachiliwa kutoka jela nchini Uingereza na anatazamiwa kuapanda kizimbani kusikiliza shauri lake la mwisho mahakamani.

Assange 2024
Julian Assange aachiwa huru kwa dhamanaPicha: George Chan/SOPA Images/picture alliance

WikiLeaks imesema Assange aliachiliwa huru kwa dhamana kutoka gerezani mjini London, alikokuwa amezuiliwa kwa miaka mitano wakati akipigana kuepuka kupelekwa nchini Marekani, ambayo ilitaka kumfungulia mashtaka kwa kuvujisha siri za kijeshi. Mke wa mtuhumiwa huyo, Stella Assange anasema atamuombea msamaha mumewe.

"Kwa uhakika, ninamaanisha nadhani kwamba hatua sahihi kwa serikali ya Marekani inapaswa kufuta kesi hiyo kabisa, ni wazi tutakuwa tunatafuta msamaha lakini ukweli kwamba kuna shitaka la hatia chini ya Sheria ya Ujasusi na kufichua habari za Ulinzi wa Kitaifa ni wazi kuwa ni wasiwasi mkubwa kwa waandishi wa habari na wanaonadika habari za usalama wa taifa kwa ujumla," alisema Stella Assange.

Julian Assange akubaliwa kupinga hukumu ya kuhamishwa Marekani

Jana Jumatatu alisafiri kwa ndege kutoka London kwenda Visiwa vya Mariana Kaskazini, eneo la Marekani ambapo atakiri shtaka moja la kula njama ya kupata na kusambaza habari za ulinzi wa kitaifa, kwa mujibu wa hati ya mahakama.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW