Assange bado yuko korokoroni
15 Desemba 2010Julian Assange mwasisi wa tovuti ya wikileaks bado yuko kizuizini. Katika dakika za mwisho mahakama ya Uswisi imepindua hukumu ya kumpatia dhamana muasisi huyo wa tovuti ya Wikileaks. Kutokana na hatua hiyo kumekuwa na hali ya malalamiko makubwa kutoka upande wa mawakili na waungaji mkono wa Assange.
Wanafanya kila wanaloweza ili kuendelea kumuweka Assange jela. Na hii inakuwa sasa kama kesi ya mchezo wa kuigiza, na tutakuwa mahakamani tena katika muda wa saa 48.
Kwa hivi sasa mahakama kuu ya Uingereza na Wales inajaribu kuangalia , iwapo dhamana hiyo itaendelea kutumika. Mahakama ya Uingereza mjini London katika eneo la Westminster, iliamua hapo kabla , kwamba mwasisi huyo wa tovuti ya Wikileaks , hapaswi kuachiliwa huru, hadi kesi yake itakaposikilizwa tena tarehe 11 Januari. Kuna hali pia ya kukatishwa tamaa kutoka kwa waungaji mkono wa Assange, ikiwa ni pamoja na mwongoza filamu maarufu na mwandishi habari , John Pilger, ambaye ameahidi kuendelea kupambana hadi kuachiliwa huru kwa rafiki yake huyo.
Nadhani kuna vitisho dhidi ya Julian. Kwasababu Julian amepata sasa maadui wakubwa , kutokana na sababu ambazo zinajulikana.
Pilger ni mmoja wa watu mashuhuri, ambao wanakusanya fedha kwa ajili ya dhamana ambayo ni kiasi cha pauni za Uingereza laki mbili, iwapo dhamana iliyotolewa itakubalika. Pamoja na hayo yuko pia mtengenezaji filamu Kan Loach na Michael Moore, mwandishi wa vitabu Hanif Koreishi na mwanaharakati wa haki za binadamu Bianca Jagger.
Sikubaliani na kila kitu alichofanya , lakini kile ambacho ni muhimu zaidi katika utaratibu wetu ni sheria, haki na uhuru wa kutoa maoni amesema hayo Jagger.
Uungwaji mkono wa watu mashuhuri unaathiri maoni ya umma nchini Uingereza kumhusu Assange. Wakati huo huo hata mama yake Assange, Christina kutoka Australia yuko mjini London , ili kumsaidia mwanae.
Mwandishi : Sebastian Hesse/ ZR / Sekione Kitojo
Mhariri : Mohammed Abdul Rahman