Athari za mgao wa umeme Tanzania
24 Novemba 2022Matangazo
Mamlaka nchini humo zinasema mgawo huo umesababishwa na hali ya ukame lakini wakosoaji wa mambo wanainyoshea kidole serikali kwa kushindwa kuweka vipaumbele vyake ili kuondokana na adha hiyo inayojitokeza mara kwa mara.
Kiasi cha umeme kinachoelezwa kupungua kinatajwa kufikia megawati 300 hadi 350 kwa siku.
Mkurugenzi mkuu wa shirika la umeme Tanzania TANESCO Maharage Chande amesema kiwango cha maji katika maeneo kama Kihansi, Bwawa la Mungu na maeneo mengine kipo chini mno.
Kwa maana hiyo hali ya mgawo huo huenda ukaandeelea kuathiri wengi hadi mwishoni mwa mwezi ujao wa Disemba ingawa shirika hilo linasema limeweka mipango kadhaa kurejesha uzalishaji wa umeme.