Athari za tumbaku ni tele kwenye mazingira: ripoti ya WHO
31 Mei 2022Kulingana na takwimu kwenye ripoti hiyo ya shirika la Afya Duniani, WHO, kuhusu madhara ya tumbaku, kila mwaka uzalishaji na matumizi ya tumbaku husababisha vifo vya watu milioni nane ulimwenguni kote.
Huchangia kukatwa kwa miti milioni 600 kila mwaka, hekari 200,000 za ardhi kutumika, pamoja na tani bilioni 22 ya maji. Isitoshe huzalisha takriban tani milioni 84 ya hewa ukaa angani, hali inayochafua pakubwa sayari yetu dunia.
Ripoti hiyo ambayo imechapishwa Jumanne, siku ya kuhamasisha kuhusu madhara ya tumbaku kote ulimwenguni, imetahadharisha kuwa hewa chafu kutokana na uzalishaji wa tumbaku na usafirishaji wake, ni sawa na moja juu ya tano ya hewa ukaa ambayo hutolewa na sekta ya ndege za usafirishaji kila mwaka, dhihirisho kwamba sekta hiyo inachangia ongezeko la joto ulimwenguni.
Uchafuzi wa vichujio vya sigara katika mazingira
Kila mwaka, takriban vipande trilioni 4.5 vya sigara huishia kwenye mito na bahari, sakafuni, ardhini na kwenye fukwe. Shughuli za kuokota taka za sigara katika mazingira yetu ni mzigo ambao raia wa kawaida walipao ushuru, hulazimika kugharamia, badala ya sekta hiyo yenyewe.
Ripoti ya WHO imetoa wito kwa mataifa kuiwajibisha sekta ya tumbaku kuhakikisha inabeba jukumu la kusafisha taka za bidhaa hiyo.
Imependekeza pia vipande vya sigara vinavyotumika kama vichujio vipigwe marufuku, ikisema vina vipande vidogovidogo vya plastiki na huchangia pakubwa katika uchafuzi wa mazingira. Licha ya hatari hizo, faida za tumbaku kiafya bado hazijathibitishwa.
Athari ya tumbaku kwa wakulima
Kwa upande mwingine, wakulima wa tumbaku huathiriwa na magonjwa yanayotokana na hewa ukaa au athri za kemikali aina ya nikotini ambayo huingia mwilini kupitia ngizi zao.
Kampuni ya tumbaku yatuhumiwa kuwahujumu washindani wake Afrika
Kulingana na Krech, inakadiriwa kwamba wakulima wanaoshughulika na tumbaku kila siku, nikotini inayotokana na sigara 50 huingia mwilini mwao kila siku. Amesema hali hii inatia wasiwasi sana hususan kwa Watoto wanaohusishwa kwenye kilimo cha tumbaku.
"Hebu fikiria, mtoto mwenye umri wa miaka 12 anakua katika mazingira ambapo yuko sawa na anayevuta sigara 50 kila siku,” amesema Krech.
Nchi masikini huongoza kuzalisha tumbaku; WHO
Mara nyingi, kilimo cha tumbaku hufanywa katika mataifa masikini. Katika nchi hizo, mashamba ya tumbaku hayapati maji ya kutosha.Ripoti imeeleza kuwa kinachosikitisha ni kwamba wakulima huendeleza kilimo hicho badala ya mazao muhimu kiafya. Wanawake wengi Tanzania watumia tumbaku
Kuhusu madhara yake kwenye misitu, kilimo cha tumbaku huchangia asilimia tano ya uharibifu wa misitu ulimwenguni kote na pia huchangia pakubwa kuangamia kwa vyanzo muhimu vya maji.
Vyanzo: DPAE, AFPE