1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ATHENS: Maelfu ya watu waandamana kupinga vyuo vikuu vya kibinafsi nchini Ugiriki.

18 Januari 2007

Maandamano yameendelea mjini Athens, Ugiriki ambapo waandamanaji wameteketeza magari na kukabiliana na polisi wa kuzima ghasia.

Maandamano hayo yameandaliwa na wanafunzi wanaopinga vyuo vya kibinafsi kuruhusiwa kuanza kufundisha nchini humo.

Ghasia hizo zilizuka tangu jana wakati maelfu ya waandamanaji walipokuwa wakielekea bungeni ambako wabunge walikuwa wakijadili suala hilo.

Nje ya jengo la bunge, vijana waliwavurumishia mawe polisi huku polisi naowakiwarushia gesi ya kutoa machozi.

Waandamanaji hao wanadai hatua hiyo itasababisha gharama ya masomo kupanda hadi ya watu maskini kushindwa kuyagharamia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW