1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ATHENS:Watumishi wa serikali na wafanyikazi nchini Ugiriki wagoma

24 Juni 2005

Watumishi wa serikali pamoja na wafanyikazi nchini Ugiriki wamefanya mgomo wa kitaifa na kulemaza shughuili zote za mji mkuu Athens.

Wafanyikazi hao wamegoma kulalamikia malipo ya Over time na mpango wa serikali wa kutaka kuufanyia mageuzi mpango wa bima ya kijamii.

Maelfu ya watu iliwabidi kutembea kwa miguu hadi kazini kufuatia ukosefu wa magari ya usafiri.

Safari za ndege 150 nyingi zikiwa za kuelekea visiwani mwa nchini hiyo zilisimamishwa.

Serikali ya Ugiriki mapema wiki hii ilitangaza nia yake ya kutekeleza mageuzi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW