1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ATLANTA : Mtuhumiwa wa ubakaji afyatuwa risasi mahkamani

12 Machi 2005

Msako mkubwa unafanyika nchini Marekani kwa mtu yaliyeuwa watu watatu na kukimbia kwenye mahkama ya Atlanta hapo Ijumaa.

Mtuhumiwa huyo wa mauaji Brian Nichols alikuwa akishtakiwa katika kesi ya kubaka na alinyakuwa bunduki ya afisa wa polisi wa kike na kufyatuwa risasi mahkamani kabla ya kukimbia. Polisi imesema hakimu aliyekuwa akisimamia kesi hiyo na mwandishi wa mhakama waliuwawa hapo hapo wakati naibu liwali alikufa baadae kutokana na majeraha.

Msako huo umezagaa hadi kwenye majimbo kadhaa ya kusini mashariki huku ujumbe wa eloktoroniki ukimuelezea mtuhumiwa huyo pamoja na gari alilotoroka nalo ukiwa umewekwa katika barabara kuu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW