1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Atletico waguchia kuelekea mwishoni mwa msimu

26 Aprili 2021

Atletico Madrid wanazidi kuteteleka katika azma yao ya kutaka kuwa mabingwa wa La Liga. miamba hao walifungwa na Athletic Bilao 2-1 Jumapili.

Atletico Madrid v Bayern Munich | Torjubel zum 1:0 durch Joao Felix (Atletico Madrid, 7)
Picha: Benjamin Soelzer/Eibner/imago images

Mnamo mwishoni mwa mwezi Januari Atletico walikuwa pointi kumi mbele katika uongozi wa ligi hiyo ya Uhispania ila kwa sasa uongozi huo umepunguzwa hadi pointi mbili tu na walio nyuma yao ni mahasimu na majirani zao Real Madrid.

Barcelona wao wanaishikilia nafasi ya tatu wakiwa na pointi 71 sawa sawa na Real Madrid ila Madrid wamewazidi kimabao ndiposa wako juu kwenye msimamo.

Mwezi Mei Atletico watakuwa wanawatembelea Barcelona uwanjani Camp Nou katika mechi inayodaiwa kwamba itaamua ni nani atakayeebuka bingwa wa Uhispania msimu huu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW