1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AU yaijadili migogoro barani Afrika

2 Julai 2009

Mkutano wa viongozi wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika uliyoanza jana,leo unaangia siku pili huku wakiwa na Mazungumzo ya kina kuhusu migogoro inayoligubika bara hilo ukiwemo ule wa Somalia.

Kikao cha 13 cha AU nchini LibyaPicha: AP



Mkutano huo katika mji wa Libya wa Sirte unaongozwa na Mwenyekiti wa mpya wa Umoja wa Afrika,Kiongozi wa Libya Moamer Ghadaf ambae anashinikiza ajenda ya Afrika kuwa na Serikali moja.


Baada ya kufunguliwa mapema mkutano huo uliendelea kwa siri mpaka jana usiku ambapo miongoni mwa mambo yalichukua nafasi kubwa kwa siku hiyo ni kukuza sekta ya kilimo Barani Afrika.


Nusu ya viongozi wa nchi Wanachama wa Umoja huo wanahudhuria huku Misri na nchi zinazoongoza kwa utajiri wa mafuta kama Nigeria na Angola zikiwa hazishiriki.


Wapiganaji wa kiislamu MogadishuPicha: AP

Mazungumzo haya ya leo sasa yanageukia katika uwanja wa siasa ambapo masuala yatakayofuatiliwa kwa kina ni migogoro inayolizonga bara la Afrika bila kulipa kisogo lile la Somalia amblo tayari AU imepeleka askari 4300.


Wanamgmabo wa Kiislam walianzisha mapambano mapya nchini humo mapema mwezi mei dhidi ya Serikali ya mpito inayoungwa mkono na Jumuiya ya Kimataifa.


Somalia kwa hivi sasa kumekuwa na kibarua kigumu kwa Walinzi wa Amani ambapo miongoni mwa majukumu makubwa ni kumlinda Rais wa nchi hiyo pamoja na maeneo muhimu kama Bandari na Uwanja wa Ndege vinaendelea kuwa huru.


Mwenyekiti wa Kamisheni wa Umoja wa Afrika Jean Ping amesema hali ilivyo nchini Somalia inaweza kurudisha taifa hilo katika zama za kutotawalika.


Amesema kutokana na nchi hiyo ilivyo Kijiografia na mambo yakiwa mabaya kutaongeza hali ya kuwa kituo cha vitendo vya uhalifu vikiwemo ugaidi na uharamia.


Somalia na nchi tano jirani zimeomba kwa Umoja wa Afrika Walinzi wengine wa Amani elfu 4.


Nchi za Sierra Leone,Nigeria na Malawi ndizo zinazoonekana kuwa tayari kutoa wanajeshi wao ingawa kwa umoja wa Afrika haijawa wazi kama una hamasa ya kuongeza idadi ya Walinzi hao endapo mambo yataendelea kuwa mabaya.


Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameahidi kutoa vikosi zaidi kwa SomaliaPicha: AP

Tayari Rais Yoweri Museveni alisema nchi yake itakua atayari kuongeza idadi ya wanajseshi wake walioko Somalia, pindi Jumuiya za kimataifa na hasa Umoja awa Afrika na Umoja wa mataifa zitakubali kutoka fedha na vifaa kwa ajili ya shughuli hiyo.


Umoja huo umeanza kuchukua hatua katika baadhi ya masuala muhimu ambapo jana uliondolewa kikwazo Mauritania baada ya kutangaza kufanya uchaguzi wa Kidemokrasia tarehe 18 mwezi huu.


Kiongozi aliyendolewa madarakani nchini Madagascar Mark Ravalomanana ambae pia Jumiya ya Kimataifa inamtabua kuwa kiongozi halali wa Kisiwa hicho anashiriki katika mkutano huo unatarajiwa kumalizika kesho.


Mwandishi:Sudi Mnette-AFPE

Mhariri:Abdul-Rahman


Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW