1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AU yaitaka EU kuondoa vikwazo dhidi ya Shadary

Sekione Kitojo
27 Novemba 2018

Baraza la Usalama na amani la Umoja wa Afrika limeutaka Umoja wa Ulaya kuondoa vikwazo dhidi ya Emmanuel Ramazani Shadary ambaye ni mgombea urais wa chama tawala DRC.

Äthiopien AU-Gipfel in Addis Adeba
Picha: Getty Images/AFP/M. Tewelde

Baraza  la  Usalama  na  amani  la  Umoja  wa  Afrika limeutaka  Umoja  wa  Ulaya  kuondoa  vikwazo  dhidi  ya chaguo  la  mrithi  wa rais  wa  Jamhuri  ya  Kidemokrasi  ya Congo  Joseph Kabila chini  ya  mwezi  mmoja  kabla  ya uchaguzi  wa  kihistoria  nchini  humo.

Mgombea  wa  chama  tawala  Emmanuel Ramazani Shadary ambaye ni waziri wa zamani wa ndani,  aliwekewa vikwazo  na  Umoja  wa  ulaya  mwaka  jana  kwa  kuzuwia hatua  za  uchaguzi  pamoja  na  ukiukaji  mwingine  wa haki  za  binadamu. 

Taarifa  ya  pamoja  ya  Umoja  wa  Afrika, bila  ya  kumtaja Shadary, imesema  kuondolewa  kwa  vikwazo  kutasaidia kuelekea  katika  uchaguzi  huru, wa  haki, unaoaminika na wa amani  nchini  Congo.

Taifa  hilo  lenye  utajiri  mkubwa  wa  madini  la  Afrika  ya kati  hapo  Desemba  23  linakabiliwa  na  kile  ambacho huenda  ni  mabadiliko  ya  kwanza  ya  madaraka  kwa amani,  na demokrasia.

Wapinzani  wanahofu  kwamba  Kabila, ambaye ameitawala  nchi  hiyo  tangu  mwaka  2001, ataendelea  na madaraka  nyuma  ya  pazia  iwapo  Shadary  atashinda.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW