AU yakosoa mauaji yanayofanywa na ADF Mashariki mwa Kongo
17 Juni 2024Mwenyekiti wa Halmashauri kuu ya Umoja huo Moussa Faki Mahamat, amesema amesikitishwa na mauaji hayo yaliyosababisha mauaji ya wengi huku akitoa wito kwaserikali ya Kongo na serikali za kikanda kujaribu kutafuta njia za haraka za kudhibiti kitisho cha ugaidi katika eneo hilo la maziwa makuu.
Soma pia:Uganda yakanusha vikali kuwaunga mkono waasi wa M23
Amesema Umoja wa Afrika unaendelea kujitolea kusaidia mataifa ya ukanda huo kupambana dhidi ya kitisho hicho. Mashambulizi hayo yanadaiwa kufanywa na kundi la wanamgambo la ADF linalodaiwa kutokea nchini Uganda.
Tangu mwishoni mwa mwaka 2021, jeshi la congo likishirikiana na la Uganda wamefanya operesheni ya pamoja dhid ya kundi hilo katika mkoa wa Kivu Kaskazini na mkoa jirani wa Ituri lakini wameshidwa kuziwia mashambulizi yanayofanywa na ADF dhidi ya raia.