1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Augsburg yaichapa Bayern derby ya Bavaria

Josephat Charo
19 Novemba 2021

Katika matokeo ya kushangaza mabingwa watetezi wa Bundesliga, Bayern Munich, wametandikwa 2-1 ugenini Augsburg na kudhihirisha ule msemo usemao "Jogoo wa shamba hawiki mjini".

Fußball Bundesliga FC Augsburg v Bayern München | Torjubel 1:0
Picha: Sebastian Widmann/Getty Images

Bayern Munich wamefungwa 2-1 na majirani zao wa Bavaria Augsburg Ijumaa katika matokeo yanayoweza kushuhudia uongozi wao wa alama nne kileleni mwa ligi ukipunguzwa kwa alama tatu katiak saa 24 zijazo.

Katika mechi ya derby ya Bavaria, Augsburg waliongoza 2-0 kutoka kwa mabao ya Mads Pedersen na Andre Hahn baada ya dakika 35 wakati Bayern walipofanikiwa kurudisha moja dakika ya 38 kupitia mshambuliaji wao matata Robert Lewandowski.

Bayern wanabaki kileleni mwa Bundesliga baada ya kupoteza mechi yao ya pili ya msimu lakini Borussia Dortmund wanaweza kupunguza mwanya kati yao iwapo wataipiku Stuttgart Jumamosi.

Augsburg wamefanikiwa kujinasua kutoka eneo la hatari la kushuka daraja na kuipita Stuttgart kwa kupata ushindi wa tatu wa msimu, ambao pia ulikuwa ushindi wa tatu dhidi ya Bayern katika mapambano 21 ya ligi, wakitoka sare mara mbili na kupoteza mechi 16 katika michuano hiyo.

dpae

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW