1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Austin amrai Trump kutoacha kuisaidia Ukraine dhidi ya Urusi

10 Januari 2025

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin ameushinikiza utawala ujao wa Donald Trump kutokata tamaa katika vita vya Ukraine dhidi ya Urusi.

Mkutano wa Ramstein kuhusu vita vya Ukraine | Austin na Zelenskiy
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin (kwenye skirini) na rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy wakizungumza kupitia kiunganishi cha vidio wakati wa mkutano wa mawaziri wa ulinzi kwenye kambi ya jeshi la Marekani ya Ramstein nchini Ujerumani.Picha: UKRAINIAN PRESIDENTIAL PRESS/REUTERS

Akizungumza katika mkutano wa kundi la mataifa linaloiunga mkono Ukraine, katika kambi ya jeshi la Marekani nchini Ujerumani, Lloyd ameonya kuwa kusitisha msaada wa kijeshi sasa, kutasababisha uchokozi zaidi, machafuko na vita.

''Ni juu ya utawala ujao kufanya maamuzi yao yenyewe. Tunataka kuhakikishiwa kuwa tumefanya kila tuwezalo kuhakikisha tunaendelea kutoa msaada, na wanaweza kuchagua upande wowote wanaotaka kuufata,'' alisema Waziri Austin.

Soma pia: Zelensky: Kurejea kwa Trump ni ukurasa mpya kwa dunia

Wakati huo huo, Trump amesema maandalizi ya kukutana na Rais wa Urusi, Vladimir Putin yanaendelea. 

Trump amesema katika mkutano wao watavizungumzia vita vya Ukraine, ingawa taarifa zaidi kuhusu mazungumzo hayo ya ngazi ya juu bado hajizaamuliwa. 

Ukraine ina wasiwasi kwamba Trump atakapoingia rasmi madarakani, misaada ya Marekani itapunguzwa sana.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW