1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Haki sawaAustralia

Australia kutangaza kura ya maoni kutambua jamii ya asili

30 Agosti 2023

Waziri Mkuu wa Australia leo anatarajiwa kutangaza tarehe ya kufanyika kwa kura ya maoni ya kihistoria ya kubadilisha katiba ili kuwatambua watu wa jamii ya asili wa nchi hiyo, japo uungwaji mkono wa kura hiyo umepungua.

Kiongozi wa jamii ya watu wa asili wa Aboriginal
Kiongozi wa jamii ya watu wa asili wa Aboriginal Picha: Asanka Ratnayake/Getty Images

Raia wa Australia wataulizwa iwapo wanaunga mkono kubadilishwa kwa katiba na kujumuisha kile kilichoitwa "Sauti kwa Bunge," kamati ya watu wa jamii ya asili ili kulishauri bunge juu ya masuala yanayoathiri watu wa jamii ya Aboriginal na wale wa visiwa vya Torres Strait.

Mabadiliko yoyote ya kikatiba nchini Australia yanahitaji kura ya maoni ya kitaifa.

Nchi hiyo haina mkataba wa aina yoyote na watu wake wa asili ambao ni asilimia 3.2 tu ya idadi jumla ya watu milioni 26 nchini humo na aghalabu huishi katika umaskini mkubwa.

Jamii hizo za watu wa asili pia hawajatajwa kwenye katiba licha ya kuishi Australia kwa zaidi ya miaka 60,000.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW