UgaidiAustralia
Australia kuweka sheria kali zaidi ya umiliki wa silaha
15 Desemba 2025
Matangazo
Washambuliaji waliwauwa watu 15 kwenye Ufukwe wa Bondi mjini Sydney wakati wakiadhimisha sikukuu ya Kiyahudi ya Hannukah. Washambuliaji walikuwa baba na mwanawe wa kiume. Baba mwenye umri wa miaka 50 aliuawa kwenye eneo la tukio baada ya kupigwa risasi na polisi, huku mwanawe mwenye umri wa miaka 24 akitiwa nguvuni baada ya kujeruhiwa.
Tukio hilo lililolaaniwa na viongozi mbalimbali duniani lilitajwa kama shambulizi la kigaidi, huku Waziri Mkuu wa Australia, Anthony Albanese, akitangaza kuwa bendera zitapepea nusu mlingoti kuomboleza mauaji hayo.