1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAustralia

Australia kutoa msaada wa dola bilioni 10 kwa ajili ya Gaza

23 Septemba 2024

Serikali ya Australia imesema hivi leo kuwa itatoa msaada wa kibinaadamu wa dola milioni 6.8 kwa Gaza ambayo inaendelea kushuhudia vita kati ya Israel na kundi la Hamas.

Penny Wong,Waziri Mkuu wa Australia
Waziri Mkuu wa Australia Penny Wong amesema serikali yake itatoa msaada wa dola bilioni 10 kwa ajili ya watu wa GazaPicha: AAP/dpa/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia Penny Wong amesema ufadhili huo utatumiwa kama msaada wa kuokoa maisha kupitia mashirika ya Umoja wa Mataifa ya UNICEF na UNFPA, hasa kwa kutoa kipaumbele kwa wanawake na wasichana.

Wakati huo huo, mapigano yanaendelea huko Gaza na wizara ya afya inayodhibitiwa na Hamas imesema kufikia sasa Wapalestina zaidi ya 41,450 wameuawa na wengine zaidi ya 95,870 wamejeruhiwa tangu kuanza kwa vita hivyo Oktoba 7 mwaka jana.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW