1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Australia kudhibiti mitandao ya kijamii kwa watoto

21 Novemba 2024

Serikali ya Australia imewasilisha muswada bungeni wa kupiga marufuku mitandao ya kijamii kwa watoto walio chini ya miaka 16, ambao unaweka faini ya hadi dola milioni 32 kwa ukiukaji.

Mitandao ya kijamii ya kampuni ya Meta
Mitandao ya kijamii ya kampuni ya MetaPicha: Jens Büttner/dpa/picture alliance

Serikali ya Australia imewasilisha muswada bungeniwa kupiga marufuku mitandao ya kijamii kwa watoto walio chini ya miaka 16, ambao unaweka faini ya hadi dola milioni 32 kwa ukiukaji.

Mfumo wa uthibitishaji wa umri, kama biometriki, utatumika kutekeleza sheria hii, ambayo ikipitishwa, itakuwa miongoni mwa kali zaidi duniani.

Waziri Mkuu Anthony Albanese amesema hatua hiyo inalenga kulinda watoto na kuhimiza kampuni za mitandao kuboresha mifumo yao. Chama kikuu cha upinzani cha Liberal kinatarajiwa kuunga mkono muswada huo, lakini wataalamu wanaonya kuwa sheria hiyo inaweza kuwaweka vijana katika mitandao isiyo salama, huku serikali ikisisitiza kuwa lengo ni kuwalinda watoto.