1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Austria kupata serikali ya kwanza ya mrengo mkali ya kulia?

7 Januari 2025

Chama kinachopinga wageni na kinachopigia upatu hatua ya kuiondolea vikwazo Urusi nchini Austria huenda kwa mara ya kwanza kikaunda serikali nchini humo.

Rais wa Shirikisho la Austria amempa Kickl wa FPÖ jukumu la kuunda serikali
Rais wa Austria Alexander van der Bellen (kushoto) akimpokea mgombea wa FPÖ Herbert Kickl katika kasri la Rais ambapo ambapo alimpa jukumu la kujaribu kuunda serikali.Picha: photonews.at/Imago

Juhudi za kuunda serikali mpya nchini humo bila ya chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Freedom Party zilishindikana katika siku za hivi karibuni, zaidi ya miezi mitatu baada ya chama hicho kushinda uchaguzi wa bunge.

Soma pia: Chama cha mrengo wa kulia chashinda Austria

Rais Alexander Van der Bellen jana alimpa jukumu kiongozi wa chama cha Freedom Herbert Kickl kuunda serikali ya mseto katika kipindi cha wiki au miezi kadhaa ijayo.

Chama hicho kiliundwa mnamo mwaka 1956 na wafuasi wa zamani wa utawala wa Manazi na katika kipindi cha miongo kadhaa kimekuwa nguvu kubwa ya kisiasa nchini Austria.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW